Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla ameonesha kutoridhishwa na kauli ya Waziri wa Mazingira, January Makamba akiieleza TANAPA kuwa hawawezi kuanza utaratibu wa kutumia magari maalumu ya umeme (Cable Cars), kwa ajili ya watalii wanaotembelea mlima Kilimanjaro.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri Kigwangalla amehoji baadhi ya maswali kwenda kwenye mamlaka ya mazingira, akieleza kuwa watu hao wamekuwa wakishiriki zaidi kwenye makongamano na si uhalisia wa kulinda mazingira.

“Hivi kuna nchi ngapi zimeweka Cable Cars kwenye milima yake?, hizi haziharibu mazingira?, Cable inapita juu inaharibu mazingira gani?. Zaidi ya hekari 350,000 za misitu zinapotea kila mwaka nchini, ipi ni hatari kubwa?, watu wa mazingira wamechukua hatua gani zaidi ya makongamano tu?”, amesema Kigwangalla.

Hivi karibuni wakati TANAPA ilieleza mpango wake wa kuja na namna mpya ya usafiri kwa watalii wanaotaka kwenda kutembelea mlima Kilimanjaro, ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba alisema kuwa suala hilo haliwezi kufanyika mpaka pale NEMC watakapo thibitisha.

“Inabidi watu wa Mazingira tupitishe na kutoa cheti kwanza kabla hawajaanza. Na tutafanya ‘studies’ ili kujua madhara kwa mazingira na uthabiti wa ‘mitigation measures”, aliandika Makamba katika ukurasa wake wa kijamii

Kundi la Haki za Binadamu lamlima barua Nicki Minaj asifanye tamasha Saudi Arabia
Video: Mnada mali za Mbowe waacha deni, Kaka yake Lissu ajitenga na uchaguzi mdogo