Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kutumia mbinu mbadala kupambana na corona ikiwemo ile ya kujifukiza.

Amesema kuwa endapo watanzania watatumia njiaza asili bila ya kuona aibu huenda Tanzania ingepunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya Virusi ya Corona.

Corona Afrika kusini: wagonjwa wapya 354 ndani ya siku moja, vifo 10

“Tusisite kutumia njia mbadala ambazo zitaweza kutusaidia katika janga hili la corona, usione aibu jifukize, kule kwetu tunasema Mtu unamuweka nyungu, watu wasione aibu piga nyungu kwelikweli na hii utaratibu wa nyungu upo katika makabila mbalimbali” amesema Jafo

Aidha amewataka watanzania kula matunda kwa wingi ili kuongeza vitamini katika miili yao za kupambana na magonjwa ya mlipuko ambapo amesisitiza kuendelea kufuata maelekezo ambayo wataalamu wa afya wanatoa.

Corona Afrika kusini: wagonjwa wapya 354 ndani ya siku moja, vifo 10

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro apata maambukizi ya corona, azungumza

Bilo: Balama aongeze juhudi
Paris Saint-Germain yakabidhiwa ubingwa 2019/20