Waziri wa Kilimo,  Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba  amekwepa mtego uliokuwa umewekwa na Rais Dkt. Magufuli, mara baada ya kufanya ziara kikazi mkoani Tanga.

Tizeba amekwepa mtego huo mara baada ya kutekeleza agizo la kutoa hati kwa ya kiwanja cha Kiwanda cha Maziwa cha Tanga Freshi kilichopo jijini Tanga.

Aidha, amekwepa kiunzi hicho cha kuungana na wenzake waliotumbuliwa tangu Rais Dkt. Magufuli aingie madarakani.

Akiwa ziarani Tanga, Rais Magufuli alimwagiza Dkt. Tizeba kuhakikisha mwekezaji huyo anapewa hati hiyo ndani ya wiki moja vinginevyo atachukua maamuzi meengine.

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli alishangazwa na Waziri huyo kutofika katika kiwanda hicho na kutatua matatizo hayo.

Majina ya watuhumiwa sugu wa uporaji yaanikwa
Video: Mtoto wa mgombea TFF ashikwa chooni akitaka kutoa rushwa kwa wajumbe Dodoma

Comments

comments