Zikiwa zimepita siku kadhaa baada ya kutolewa rai bungeni ya kuwataka wananchi kupunguza ulaji wa nyama, ili kukabiliana na ongezeko la udhibiti wa hewa ya ukaa nchini Uingereza, waziri wa mazingira nchini humo Claire Perry, amepinga vikali hoja hiyo na kuwataka wananchi kula nyama watakavyo.

Hoja hiyo ilitolewa na wanasiasa walio ungana na wanamazingira, kwa kusisitiza kuwa ili kudhibiti hewa ya ukaa lazima kampeni ya kupunguza ulaji wa nyama ifanyike.

Aidha, wanasayansi nchini Uingereza wamebaini kuwa ili kupunguza hewa ya ukaa duniani ni lazima jamii ipinguze ulaji wa bidhaa zitokanazo na nyama, pia wanaungwa mkono na wana harakati ambao wanasisitiza matumizi madogo ya kula nyama.

Hata hivyo, jambo hilo linapingwa vikali na waziri wa mazingira ambaye anasisitiza kulima mbogamboga kwa wingi na kupanda miti kutasaidia kutatua taizo hilo lakini sio kuacha kula nyama.

Marekani yaipongeza Tanzania kwa kuvutia wawekezaji
Mahakama yapiga chini pingamizi la matokeo ya urais