Tamu ya kugawana faida katika kikundi cha ujasiriamali cha Imani Mkoani Arusha imeingia doa baada ya baadhi yao kuzimia ghafla ukumbini kutokana na taarifa ya upotevu wa zaidi ya milioni 39 zinazodaiwa kuyeyuka kwa njia ya kishirikina.

Fedha hizo zinadaiwa ziliyeyuka ndani ya sanduku la fedha nyumbani kwa mweka hazina wa kikundi hicho chenye wanachama 20.

Mmoja wa wanakikundi, Grece Magala amesema kikundi chao chenye miaka mitano tangu kuanzishwa hawajawahi kugawana faida yoyote hadi juzi walipokaa na kukubaliana kugawana faida iliyopo.

Wanakikundi hao waliambiwa fedha zimeyeyuka ndani katika mazingira ya kutatanisha jambo lililozua taharuki kwa wanachama wanawake waliokuwa wameambatana na waume zao ili kupokea gawio kwa lengo la kufanya manunuzi na mahitaji mengine ya majumbani.

Katibu wa kikundi hicho, Deogratius Seif amesema wanaendelea na ufuatiliaji na watakutana na viongozi wa kikundi kujua tatizo na watatoa taarifa kamili kuhusu upotevu huo wa fedha.

Mchakato wa kusaka tiketi AFCON 2021 waanza rasmi
Zlatan Ibrahimovic amalizana na LA Galaxy

Comments

comments