Kamati ya uchaguzi klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti wake, Boniface Lyamwike, imeweka wazi majina 19 ya wajumbe waliochukua fomu ambapo kati yao wajumbe 17 wamepita na wajumbe 2 wameenguliwa kuelekea uchaguzi mkuu wa klabu unaotarajia kufanyika Novemba 3, 2018.

Ambapo wajumbe 17 waliopitishwa ni Hussein Kitta Mlinga, Iddy Noor Kajuni, Zawadi All Kadunda, Mohamed Wandi, Selemani Harubu Said, Abdallah Rashid Mgomba, Christopher Kabalika Mwansasu, Alfred Matin Elia, Ally Suru, Mwina Mohamed Kaduguda, Said Tully, Jasmine Badar Soudy, Juma Abbas Pinto, Hamis Ramadhani Mkoma, Abubakari Zebo, Patrick Paul Rweyemamu, Asha Ramadhani Baraka.

Na wajumbe 2 walioenguliwa ni Selemani Omari Selemani na Omar Juma Mazola.

Pia taarifa ya kamati hiyo imewataja waliopitishwa katika nafasi ya Uenyekiti ni Swedy Mkwabi na Mtemi Ramadhani.

Aidha katika uchaguzi huo kwa mujibu wa katiba mpya ya mwaka 2018, mgombea wa nafasi ya Uenyekiti anapaswa kuwa na kiwango cha elimu ya Shadaha kutoka Chuo Kikuu na katika orodha ya wajumbe watano watakaopigiwa kura, mjumbe mmoja atapaswa kuwa na shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu huku wengine wakiwa na kiwango cha elimu ya kidato cha nne.

Na katika hao wajumbe watano mjumbe mmoja anapaswa kuwa mwanamke ili kuleta usawa wa kijinsia katika uwajibikaji wa kazi za klabu.

Mbatia ailaumu sana serikali sakata la Mv Nyerere kuzama
Miili 94 yaopolewa ajali ya Mv Nyerere