Huku familia inaomboleza kifo cha mfanyabiashara tajiri, Reginald Mengi aliyefariki mapema mwezi huu, watu wasiofahamika wameiba vito kama vile mikufu ya dhahabu, vifaa vya thamani, laptop na fedha taslimu katika nyumba ya mjane,  Jacquleine Mengi na nyumba ya kifahari ya familia ya Regnald Mengi ambako amezikwa.

Msemaji wa familia hiyo Benson Mengi amesema kwa sasa hawawezi kuzungumzia jambo hilo kwa kuwa bado uchunguzi unaendelea.

”Bado uchunguzi unaendelea alisema, Benson ambaye ni mtoto wa mdogo wake Reginald Mengi anayeitwa Benjamin Mengi”.

Kamanda wa polisi mkoa Kilimanjaro, Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la wizi kwenye nyumba za kifahari za marehemu Mengi na amedai kuwa tukio hilo limefanyika na watu wanaodaiwa kuwa wa ndani ya familia kwani taarifa zinazonyesha walitokea jijini Dar es salaam.

”Ni kweli nyumbani kwa Mengi kumeibiwa amesema Kamanda” amesema Kamanda.

Hata hivyo tayari jeshi la polisi linawashikilia watu wawili ambao majina yao hayakuwekwa wazi wakidaiwa kuhusika na tukio hilo la wizi.

Kamanda ameongezea;

”Kumetokea watu mchanganyiko familia ile watu wengi walikuwa hawafahamiani matokeo yake kila mtu anasema mimi na kila mtu anaingia mahali ambako hausiki matokeo yake ni wizi” amesema kamada’

Aidha, Mengi (77) ambaye alikuwa anajihusha na uchimbaji wa madini na kumiliki vyombo vya habari kama vile televisheni, magazeti, pia alikuwa ni mmiliki wa viwanda vya vinywaji baridi, alifariki dunia Mei 2 akiwa Dubai, Falme za kiarabu na kuzikwa kwao Moshi Machame Kijiji cha Nkuu mkoani Kilimanjaro.

Chanzo Mwananchi

Fahamu dalili, matatizo yatokanayo na dengue
Maeneo hatari kwa Dengue yatajwa Dar, idadi ya wagonjwa yapaa