Klabu ya Southampton ipo kwenye mashaka ya kuwapoteza wachezaji wawili muhimu katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi ambacho kimesiliwa na siku chache kabla ya kumalizika Septemba mosi.

Southampton ambayo msimu uliopita ilionyesha upinzani mkali katika michezo ya ligi ya nchini England, imekua ikitazamwa kwa macho mawili kama mbadala wa kuwatoa wachezaji ambao wanakwenda kuziba nafasi muhimu kwenye klabu nyingine za nchini humo.

Taarifa zinadai kwamba Man Utd baada ya kumkosa mshambuliaji wa FC Barcelona, Pedro Rodríguez wamehamishia hasira zao kwa mshambuliaji wa The Saints ambaye ni raia wa nchini Senegal Sadio Mane.

Mane amekua akiiongoza vyema safu ya ushambuliaji ya klabu ya Southampton, na msimu uliopita alionekana kuwa chachu ya kuipatia ushindi klabu hiyo hususan katika michezo muhimu.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, aliifungia Southampton mabao 10 katika michezo  32 aliyocheza na amekua mchezaji wa kwanza katika ligi ya nchini England kufunga mabao matatu (hat-trick) katika muda wa sekundu 176, wakati wa mchezo dhidi ya Aston Villa, msimu uliopita ambapo The Saint waliibuka na ushindi wa mabao 6-1.

Mane alijiunga na klabu ya Southampton, kwa ada ya paund million 10, akitokea nchini Austria alipokua akiitumikia klabu ya Red Bull Salzburg.

Mchezaji mwingine ambaye yu njiani kuihama Southampton ni kiungo kutoka nchini Kenya, Victor Wanyama ambaye anahitajika kwa udi na uvumba huko White Hart Lane yalipo makao makuu ya klabu ya Tottenham Hotspurs.

Yametimia, Song Kubaki England Jumla
Kaseja Rasmi Mbeya City