Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Mkoani Njombe limepitisha na kuridhia kuwasimamisha kazi watumishi wapatao 50 waliojipatia ajira kwa njia ya udanganyifu na mtumishi mmoja aliyethibitika kuwa ni mtoro kazini.

Akitangaza mapendekezo ya Kamati Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Egnatio Mtawa amesema kuwa hayo ni mawazo ya baraza la madiwani lilojigeuza kuwa kamati ili kuweza kujadili juu ya jambo hilo.

“Kamati imefikisha mapendekezo kwenye baraza kwamba wtumishi wapatao 60 watendaji wa vijiji, Afisa Mifugo mmoja, Fundi sanifu mmoja na madreva wanne wathibitishwe kwenye ajira zao lakini pia kamati imependekeza watumishi wapatao 50 waliojipatia ajira kwa njia ya udanganyifu,na mtumishi mmoja ambaye amethibitika kuwa na utoro sugu kazini hao wote wafukuzwe kazi,”amesema Mtawa

Aidha, wakati huo huo Mtawa ameongeza kuwa baraza limeweza kuunda tume ya uchunguzi wa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri kupitia kwa watendaji wa vijiji na watendaji wa kata katika halmashauri ya wilaya hiyo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa baraza limewateu, Jonson Mbalizi kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete, Abraham Okoka mjumbe wa kamati ya fedha na Atilio Ng’ondya diwani wa kata ya Mpungi kuwa  wajumbe wa tume iliyoundwa kuchunguza masuala ya utendaji kazi.

 

Mlinga amuomba JPM ashtukie mtego wa Chadema, amgusa Masoud Kipanya
Wadau wa Soka wamlilia Sala baada ya mwili wake kupatikana