Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani leo Juni 26, kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupambana na matumizi na biashara ya dawa za kulevya, ikiwa ni nchi mwanachama wa umoja wa mataifa.

Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa mkoani Tanga yakiwa na kauli mbiu “Waathirika wa dawa za kulevya wana haki ya kupata huduma za afya” lengo likiwa ni kuikumbusha jamii juu ya uelewa wa wimbi la biashara na matumizi ya dawa za kulevya.

Kutokana na Serikali kuendelea kusimamia utoaji tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya ili kupunguza madhara yanayotokana na matumizi ya dawa hizo, na kufanikiwa kupunguza idadi ya waathirika wa dawa za kulevya katika vituo vya tiba kutoka wagonjwa 2,400 mwaka 2015 hadi wagonjwa 700 mwaka 2018.

Hali iliyosaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa waraibu wa dawa za kulevya wanaojidunga kutoka 35% mwaka 2015 hadi 18.5% mwaka 2018.

Ikumbukwe kuwa matumizi ya dawa za kulevya husababisha madhara kiafya ikiwa ni pamoja na kuchochea kuenea kwa maambukizi ya vurusi vya UKIMWI, virusi vya homa ya ini aina B na C,kifua kikuu, magonjwa ya akili pomoja na usugu wa tiba ya kifua kikuu.

 

Iran yaitaka Marekani kutii makubaliano ya mwaka 2015
Boomplay kuboresha tasnia ya muziki Tanzania

Comments

comments