Dereva wa Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia tiketi ya Chadema, John Heche amevamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na kujeruhiwa vibaya kwa mapanga.

Heche amethibitisha kuvamiwa kwa dereva wake kutokana na taarifa alizopata kupitia Katibu wake, Mrimi Zablon ambaye amekiri Dereva huyo anayefahamika kwa jina la Suez Daniel ambapo kwa sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu.

Aidha,kwa upande wa Kamanda wa Polisi Tarime, SACP Henry Mwaibambe alipotafutwa kwa njia ya simu na Mwandishi wetu amesema yupo kwenye kikao na akimaliza atatoa ripoti kamili.

Hata hivyo, mpaka sasa Dereva huyo amelazwa katika hospitali ya Bomani mjni Tarime mkoani Mara.

Kamati ya bunge yakwama kutoa ripoti ya Lissu
RC Rukwa ataka wahalifu wachomwe

Comments

comments