Jeshi la Polisi mkoa wa Mjini Magharibi, linamshikilia raia mmoja wa china na wa Zanzibar wawili wakiwa na kobe wapatao 508 kinyume na sheria.

Watatu hao Huang Xiaohua Huang(44), Makidadi Said Nangaliwe(32) mkazi wa mwera na Hassan Ramadhan Kondo (35), mkazi wa mombasa Unguja wamekutwa wamehifadhi kobe zaidi ya mia tano kwenye nyumba waliyokodisha maeneo Mombasa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Thobias Sendoyeka, amesema watuhumiwa hao wanadaiwa kuwaingiza kobe kutoka Madagascar na kuwahifadhi zanzibar na baadaye kuwasafirisha kwenda kuwauza Vietnam.

Watuhumiwa hao akiwemo raia huyo wa China Haung, aliyekutwa na hati ya kusafilia yenye namba E. 60903207, walikamatwa April 30 mwaka huu saa 8 mchana katika nyumba namba SH/MA/A/117 iliyoko maeneo ya Mombasa wakiwa na kobe hao.

Kukamatwa kwa watuhumiwa kwao kunafuatia taarifa za kiintelejensia kutoka Tanzania Bara, kwamba kuna watu wanafanya shughuli hizo, ndipo polisi kwa kushirikiana na ofisi ya maliasili wakafanikiwa kuwakamata.

Kamanda Sedoyeka amesema kwasasa watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi kwa ajili ya kukamilisha upelelezi ili kufikishwa Mahakamani.

Shamim, mumewe wakamatwa na dawa za kulevya, ‘wana mtandao wa kimataifa’
Gigy Money ataja tarehe ya kuvalishwa pete