Upepo mkali unaotokana na kimbunga Florence ambao unatishia watu wengi Marekani umeanza kupigia maeneo ya Pwani ya Mashariki ya Marekani.

Maafisa wamesema kuwa huenda mawimbi makubwa ya kutoka baharini na mvua kubwa vikaathiri maeneo ya ‘North na South Carolina’, huku kimbunga hicho kikielekea maeneo ya bara.

Upepo wa kimbunga hicho unavuma kwa kasi ya maili 100 kwa saa (155 km/h), nyumba takriban 100,000 tayari hazina huduma ya umeme huku hali ikitarajiwa kuwa mbaya zaidi.

Aidha, watu zaidi ya milioni moja katika maeneo ya Pwani North Carolina, South Carolina na Virginia wametakiwa kuyahama makazi yao.

Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo ya North Carolina mvua ya kina cha futi moja ilinyesha katika kipindi cha saa kadha, na picha zilionyesha maji yakijaa baharini na kufunika maeneo ya ufukweni.

CCM yaongoza kuwa na wasomi wengi bungeni
Serikali mkoani Simiyu kutoa ardhi bure kwa wawekezaji