Watu waliokuwa wakisafirisha miili mitatu ya marehemu iliyokuwa kwenye majeneza, wakitokea Afrika Kusini kuelekea Msumbiji wamesusa majeneza hayo mpakani.

Kwa mujibu wa O País, watu hao walichukua uamuzi huo baada ya maafisa wa uhamiaji waliokuwa mpakani kuwaeleza kuwa hawakuwa na nyaraka stahiki za kuvusha miili hiyo.

Imeelezwa kuwa watu hao waliiacha miili hiyo katikati ya barabara kwenye eneo la Ressano Garcia la Afrika Kusini.

Maafisa wa Serikali ya Afrika Kusini wameeleza kuwa majeneza hayo yaliyokuwa na miili miwili ya wanaume na mmoja wa mwanamke yamehifadhiwa katika eneo la Maputo.

O País imeripoti kuwa baadhi ya ndugu wa marehemu hao walirejea nchini kwao kutafuta baadhi ya nyaraka, na wengine walikosa sehemu ya kusubiria utaratibu huo na kujikuta wakitafuta msaada wa malazi kwa wasamalia wema.

Rafiki wa Lowassa atoa ya moyoni, ‘angenipa hata dakika moja..’
Rwanda yakanusha kufunga mpaka wake na Uganda

Comments

comments