Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewasimamisha kazi watumishi wake sita kwa makosa mbalimbali ya kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi, Abdulzack Badru alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari,

Amewataja viongozi hao waliosimaishwa kuwa ni Juma Hamisi Chagonja Mkurugenzi wa urejeshaji wa mikopo aliye sababisha hasara kwa uzembe na kushindwa kutumia majukumu yake ipasavyo kwa mujibu wa sheria.

Aidha, wengine ni Onesmo Ngitiri Laizer Mkurugenzi upangaji na ugawaji mikopo ambaye amesababisha hasara ya bilioni 7.1, John Elius Mkurugenzi msaidizi ugawaji mikopo amesababisha hasara ya bilioni 7.1,

Vile vile amewataja, Robert Kibona Mkurugenzi msaidizi wa urejeshaji mikopo, Heti Sago Mkaguzi mkuu wa ndani wa hesabu, na Chikira Habari Mkurugenzi msaidizi wa upangaji mikopo ambaye amesababisha hasara ya Bilioni 7.1

 

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Senegal
Marekani, Canada na Mexico wenyeji kombe la dunia 2026