Wasichana zaidi ya milioni 68 wako hatarini kukeketwa kufikia mwaka 2030 endapo hatua stahiki hazitachukuliwa dhidi ya vitendo hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres jana katika siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji ambao ni kinyume cha haki za binadamu na utu wa wanawake na wasichana.

Tamko la Guterres limeeleza kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 200 wanaoishi duniani wamefanyiwa ukeketaji.

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa wastani wa wanawake na wasichana milioni 3.9 wanaokeketwa kila mwaka unaweza kupanda hadi milioni 4.9 kwa mwaka endapo hatua stahiki na za haraka dhidi ya vitendo hivyo hazitachukuliwa.

Serikali na jamii kwa pamoja zimetakiwa kuhakikisha zinaweka nia na kuchukua hatua kwa vitendo na kutumia rasirimali zake kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa kuondoa ukeketaji kufikia mwaka 2030.

Barabara ya juu Tazara kukamilika kabla ya muda
Dada yake Kim Jong Un kuhudhuria Olympics Korea Kusini