Marekani imewapiga marufuku wasafiri waliokuwa nchini Brazil kuingia nchini humo katika muda wa wiki mbili, hatua ambayo imeelezwa kuwa ni mwendelezo wa juhudi za kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya corona.

Serikali ya Rais Donald Trump umezuia safari za ndege kutoka Umoja wa Ulaya, Uingereza na China.

Marufuku hiyo dhidi ya wasafiri kutoka Brazil ambayo inaanza kutekelezwa Alhamisi ijayo haiwahusu raia wa Marekani na wale wenye vibali vya kudumu vya kuishi nchini humo.

Hayo yamejiri huku Marekani ikiwa inaongoza kwa idadi ya watu waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona, ikifuatiwa na Brazil na Urusi.

Kwa mujibu wa takwimu za Chuo Kikuu cha John Hopkins, Brazil ina visa 347,000 vya maambukizi ya corona na vifo 22,000.

Madareva wa malori 200 wapimwa Corona Dar, Ummy awapa ushauri
Ajuza mwenye miaka 107 apona corona