Msanii wa muziki wa hip hop nchini Tanzanai, Young killer ameibuka na kulimwgia sifa tamasha la wasafi festival baada ya kushiriki uzinduzi uliofanyika novemba 24 mkoani Mtwara huku wasanii wengi wakipewa nafasi ya kushiriki katika tamasha hilo.

Msanii huyo ambaye alishafanya collabo na raisi wa WCB Diamond Plutnumz, amesema kuwa tamasha hilo la wasafi festival limekuwa ni ukombozi katika sekta ya burudani nchini Tanzania kwani kumekuwa na matamasha machache sana, kitu kinachopelekea wasanii kutokupata nafasi ya kuonyesha muziki wao.

“Ujio wa Wasafi Festival ni mkubwa na umekuja kitofauti sana na kiukweli tasnia yetu inahitaji vitu kama hivi kwa sababu haya ni mapinduzi makubwa kwasababu ni muda mrefu tumekuwa tukikosa matamasha,”amesema Young killer

Aidha, tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufanyika mkoani Iringa siku ya leo huku wasanii wengi wakiwa wamepata nafasi ya kuburudisha.

 

Sonara kumdai mamillioni ya pesa Young Thug
Wafuasi wa Chadema watimuliwa mahakamani

Comments

comments