Ni mtindo ambao umezuka kwa wadada wengi mjini ambapo kusuka kwa sasa sio fasheni kwa wadada wengi.

Kila kitu ni fasheni inategemea na ubunifu wa mtu na jinsi atavyopenda muonekano wake uweje mbele ya watu wanaomtazama.

Ni dhahili kuwa gharama za maisha zimepanda bei, kikawaida mwanamke nadhifu kwa mwezi anatakiwa kusuka mara tata au mara nne ili jamii inayomzunguka iendelee kumuona yuleyule akiwa nadhifu, ila kulingana na hali ya maisha kuwa ngumu swala hilo limekuwa gumu kwa wanadada wengi wenye maisha ya kawaida.

Sababu kwa hesabu za haraka kusuka nywele mtindo wa kawaida si chini ya 30,000 kwa bajeti hiyo kila mwezi utagharamika 120,000, ikiwa ni nje ya matunzo mengine ya nywele kama kuweka dawa, kununua dawa, kununua mafuta na huduma nyingine muhimu kwa matunzo ya nywele yako.

Hivyo katika kukabiliana na changamoto hiyo pamoja na changamoto ya uchumi idadi kubwa ya wanadada wamegundua mbinu mbadala ya kudumisha urembo wao bila kugharamika kiasi kikubwa cha pesa.

Kipindi hiki katika wadada kumi nane kati yao wamenyoa na wanaonekana nadhifu na wazuri wakiwa na muonekano huo wa nywele fupi.

Angalia wanawake watano ambao huwapa ujasili wanawake wengi mjini kuchukua uamuzi kuingia saluni na kukata nywele zao na kuwa ‘natural beuty’, yaani urembo asilia.

Image result for flaviana matata

  1. Mwanamitindo Flaviana Matata anafanya vizuri katika sanaa yake ya mitindo, ni mmoja kati ya wakinadada wajasiliamali wakubwa wenye mchango mkubwa katika jamii, kutokana na misaada mikubwa anayoitoa kwa jamii yenye uhitaji, Huyu mwanadada ni moja kati ya wahanga wa alali ya MV Bukoba ambapo alipotezi wazazi wake wote wawili katika ajali hiyo, hivyo kila mwaka tunapoenzi siku hiyo huikumbuka kwa kutembelea ndugu na wahanga wengine wa tukio hilo na kuwapa misaada mbalimbali kama namna ya kuwafariji.

Image result for jackline ntuyabaliwe

2. Jackline Ntuyabaliwe, amewahi kushiriki shindano la Miss Tanzania na kuchukua taji mwaka 2000 na sasa ni mke wa mfanyabiashara mkubwa Tanzania na mmiliki wa kituo cha televisheni kikubwa Tanzania IPP Media, Regnard Mengi.

Image result for faraja nyalandu

3. Faraja Nyalandu, amewahi kushiriki shindano la Miss Tanzania na kuchukua taji hilo mwaka 2004, na sasa ni Mkurugenzi na mwanzilishi wa Taasisi inayojishughulisha na kutoa elimu kupitia mtandao, Shule Direct.

Image result for amber lulu

4. Amber Lulu, huyu ni mpendezesha video ”video vixin” na sasa ni msanii wa muziki wa bongo fleva anayefanya vizuri katika ngoma zake.

Image result for tunda

5. Tunda.

 

 

 

Yanga yaichapa Stand United
Mmiliki wa shule ya 'daycare' ahukumiwa jela miaka 21