Shirikisho la soka  Barani Afrika CAF limepitisha majina manne ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kuwa makamishna wa michezo mbalimbali inayoandaliwa na CAF.

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizotoa Makamishna wanne ambayo ni idadi ya juu hakuna nchi iliyozidisha idadi hiyo ambayo ni kwa kipindi cha kutokea mwaka 2018 mpaka 2020.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF waliopata nafasi hiyo ni Makamu wa Rais Michael Wambura,Ahmed Mgoyi,Amina Karuma na Sarah Tchao.

Wambura kwa upande wake amechaguliwa kutokana na kufanya vizuri katika aiku za nyuma wakati Mgoyi amepata nafasi hiyo kwa kufanya vizuri kama mechi kamishna wa michezo ya CECAFA nao Karuma na Tchao wameipata nafasi hiyo kutokana na  mkakati wa CAF kuanza kuwajengea uwezo viongozi wanawake vijana.

Kuteuliwa kwa viongozi hao wa TFF ni muendelezo CAF kuteua viongozi wa TFF kwenye kamati mbalimbali itakumbukwa hivi karibuni Rais wa TFF aliteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya fainali za Africa kwa wachezaji wa ndani CHAN inayoendelea nchini Morocco lakini pia akiteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya ufunguzi iliyowakutanisha wenyeji Morocco na Mauritania.

NJombe Mji yashinda uwanja wa Sabasaba
Serengeti Boys kambini hadi Januari 28