Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amemtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kusimamia kwa karibu, umakini na kuongeza kasi ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga baada ya kuona kusuasua kwa ujenzi huo tangu kuanza kwake tarehe 19 Januari, 2019 ambapo wananchi walijitokeza kuchimba misingi ya majengo saba ya hospitali hiyo.

Amesema kuwa muda mwingi umepita tangu kuanza kwa ujenzi huo na ambapo hadi sasa ilistahili uwe umefikia hatua ya lenta na matokeo yake bado ipo kwenye hatua ya jamvi pamoja na changamoto zilizokuwepo na kuongeza kuwa hali hiyo inawakatisha tamaa wananchi kwa kuona jengo halipandi tangu kuanza kushiriki kwao kwenye ujenzi huo.

“Kuna haja kwa halmashauri kusimamia ujenzi huu kwa karibu kuanzia sasa hivi kasi iongezeke mara mbili hata tatu kwa ile iliyokuwepo kwasababu kuapanga matofali kwenda juu hata siku mbili au tatu unafika kwenye lenta lakini kutoka kule kwenye msingi kunahitaji uangalifu na kupanga vizuri zaidi, kwahiyo Mkurugenzi narudia tena simamia vizuri ujenzi wa hapa na kwa ukaribu zaidi,”amesema Wangabo.

Ameyasema hayo alipotembelea eneo la ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Sumbawanga inayojengwa katika Kijiji cha Mtowisa, Kata ya Mtowisa, bonde la ziwa Rukwa na kuwataka mafundi wote waliokabidhiwa kujenga majengo saba ya hospitali hiyo kuhakikisha wanafikia ngazi ya lenta ifikapo tarehe 10 Mei, 2019 na kuongeza kuwa asiyefikia hatua hiyo atawajibishwa.

Aidha, wakati akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dkt. Fani Musa amewashukuru wananchi kwa kujitolea kwao kwa kazi za songambele zilizookoa shilingi 18,600,200 ikijumuisha kazi za kuchimba misingi ya majengo na mtaro wa kupeleka maji eneo la ujenzi, kusogeza tofali na ujazaji wa kifusi kwenye majengo hayo.

Ili kukamilisha ujenzi wa majengo saba ya hospitali hiyo ambayo ni majengo ya Utawala, Kufulia, Dawa, OPD, Maabara, Mionzi na Wazazi ni matofali 84,000 yanahitaji ambapo hadi sasa matofali 70,666 yameshafyatuliwa huku shilingi milioni 496 zikiwa zimeshatumika

Kundi la ISIS limetangaza kuhusika na Mashambulizi ya Sri Lanka
LIVE: Rais Magufuli akiwa ziarani nchini Malawi