Jeshi la Polisi nchini Kenya linawashikilia wanawake 11 kwa tuhuma za kurekodi filamu za ngono na kuziuza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na Citizen, mbali na wanawake hao, polisi pia wamewakamata watu wawili waliotajwa kwa majina ya Merceline Atieno na Enock Ochieng wanaodaiwa kuwa wanamiliki tovuti yenye maudhui ya ngono ya kulipia kwa kushirikiana na kampuni ya Multi Meida Illc.

Watu hao wawili wanadaiwa kuwa ndio wanaowasimamia wanawake hao katika kukamilisha biashara hiyo haramu.

Polisi wameeleza kuwa watu hao walikamatwa baada ya askari kupata taarifa na kuvamia nyumba waliyokuwemo. Imeelezwa kuwa katika nyumba hiyo, polisi walikamata kompyuta mpakato 16, kamera kadhaa, simu za mkononi, flash na midoli ya ngono.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani Ijumaa, Julai 12, 2019 na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkuu, Florence Macharia lakini hawakutakiwa kujibu chochote.

Polisi waliiomba mahakama kuwapa siku tano ili kukamilisha upelelezi, ombi ambalo Mahakama ililiridhia.

Kama ilivyo kwa Tanzania, nchini Kenya ni kosa la jinai kwa mtu kurekodi, kuchapisha, kusambaza picha zenye maudhui ya ngono (pornography) au hata kujihusisha na biashara hiyo na sheria imetaja adhabu kali kwa watakaokutwa na hatia.

Real Madrid wathibitisha kifo cha kaka yake Zidane
Wanaotaka Kujiunga Vyuo Vya Elimu ya Juu Watahadharishwa

Comments

comments