Wananchi wa Kijiji cha Isimike Kata ya Saja wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe wamelazimika kujenga madarasa mawili na ofisi katika shule ya msingi Isimike ili kukabiliana na mlundikano wa wanafunzi katika madarasa yaliyopo.

Taarifa ya kijiji cha Isimike iliyosomwa na afisa mtendaji wa kijiji hicho, Julius Mpiluka mbele ya mbunge wa jimbo la Wanging’ombe Mhandisi, Gerson lwenge katika ziara yake ya kibunge imeeleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 14 zimetumika hadi sasa katika ujenzi huo uliofikia usawa wa lenter.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Isimike, Nichorus Kabelege amesema kuwa bado shule hiyo itaendelea kukabiliwa na upungufu wa madarasa saba katika shule hiyo baada ya kujengwa madarasa hayo mawili yanayokaribia kukamilika.

“Kwasasa baada ya kuongeza madarasa haya mawili tumekuwa na madarasa 8 kati ya 6 tuliyokuwa nayo, kwa hiyo tunaupungufu wa madarasa saba ambayo tunaendelea kuyajenga taratibu,kwa jengo hili ambalo linaendelea, tunaiomba serikali iendelea kutusaidia pamoja na kutumia nguvu ya wananchi, wahisani pamoja mheshimiwa mbunge lakini bado kunahitajika kukamilishwa kwa maana ya finishing kwa ujumla,”amesema Kabelege

Naye mbunge wa Jimbo hilo, Gerson lwenge ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa madarasa na ofisi hiyo huku akiwataka kukamilisha zoezi la upigaji mbao ili awapelekee bati zitakazotosha katika majengo hayo.

“Mmeniomba bati ya jengo hili,na mimi kwasababu nilitoa ahadi jengeni maboma,najua serikali itakuja kutupatia nguvu lakini wakati tunaisubiri serikali na mimi mbunge nitatoa hizo bati 150”amesema Lwenge

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 5, 2019
Marafiki wa Jussie Smollet wathibitisha uvamizi aliofanyiwa Chicago