Wananchi wa Kata ya Makoga Wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe wameanza ujenzi wa baadhi ya majengo ya kituo cha afya cha Makoga lengo likiwa ni kutatua baadhi ya changamoto zinazokikumba kituo hicho kilichopo katika kata hiyo ili kunusuru upatikanaji wa huduma za afya kituoni hapo.

Hatua hiyo inakuja mara baada ya kituo cha afya Makoga kukumbwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa wa hudumu pamoja na ukosefu wa gari la wagonjwa katika hicho huku jengo lililopo likiwa limechoka.

“Yaani huwa tunatafuta tu Magari kwa gharama zozote, sisi ni wakulima, hatuna kiwango kikubwa cha kukodi gari mpaka hospital kubwa, na unaweza ukafika kwenye kituo chetu hapo hata masaa mawili, matatu wakati wa usiku mpaka wakati mwingine tunaamua kutafuta mhudumu huko mitaani, na ukiangalia changamoto kweli kwetu ni nyingi,”wamesema baadhi ya wananchi

Akizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe, Ally Kasinge, Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Makoga, Betty Hamza amesema kuwa miongoni mwa changamoto zilizopo katika kituo cha afya ni pamoja na upungufu wa majengo ya kutolea huduma.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Ally kasinge ameahidi kutafuta fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa upungufu wa majengo katika kituo hicho ndani ya mwaka 2019

RPC Wankyo awatangazia kiama Trafiki wala rushwa
ICC yamuachia huru Rais wa zamani wa Ivory Coast