Wananchi wa Kijiji cha Usagatikwa Kata ya Tandara wilayani Makete mkoani Njombe wamemuomba Naibu Waziri wa Nishati, Subira mgalu kuchangia gharama za usambazaji wa nishati ya umeme ili uweze kufika mapema katika vitongoji vyao.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho wakati akiwasha Transfoma moja kati ya Tatu zinazohitajika, Subira Mgalu amemtaka mkandarasi wa usambazaji wa umeme wa REA awamu ya tatu kuhakikisha anaongeza kasi ya usambazaji na uunganganishwaji kabla awamu haijamalizika kwa kuwa mpaka sasa ni vijiji 58 pekee kati ya 96 ndivyo vimeunganishwa na umeme.

“Madhumuni makubwa nikufika hapa na kuona kinachoendelea iwe jua iwe mvua serikali hatukubali, tunachotaka mkandarasi ni kuongeza kasi kwa kuwa kazi yake bado japo hatua tunaziona,”amesema Mgalu

Aidha, Mgalu amefika katika kijiji cha Usagatikwa akiendelea na ukaguzi wa usambazaji umeme na kushangazwa kuona wananchi wa kijiji hicho wakimuomba kiongozi huyo kuwapa nafasi ya kutoa mchango wao ili wafikiwe na umeme kutokana na uhitaji mkubwa wa Nishati hiyo.

Hata hivyo, Naibu Waziri huyo amewata wananchi wa Wilaya ya Makete na Mkoa wa Njombe kwa ujumla kushirikiana na Serikali katika kutunza vyanzo vya maji kwa kuwa maji yanayotiririshwa katika Mto Luwegu, Mto Ruaha Mkuu na Mto Kilombelo na kuyapeleka katika mto Rufiji ambako ndiko ujenzi wa mradi mkubwa wa bwawa la uzalishaji umeme linajengwa.

 

Ajiua kwa kukosa ajira
Mradi mkubwa wa umeme waanzishwa wilayani Ludewa

Comments

comments