Wananchi wa Kijiji cha Igombola Kata ya Lupembe wilayani Njombe wamesema kuwa hawana Imani na Mwenyekiti wao wa kijiji anayejulikana kwa jina la Josephati Kiluka kutokana na kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo na kudai kuwa anafanya kazi kwa maslahi yake binafsi.

Wananchi hao wamesema kuwa hawana imani na mwenyekiti huyo baada ya kubadili mahali ambapo miradi ya maendeleo ilipokuwa imepangwa kufanyika na kupeleka sehemu ambayo ni tofauti na makubaliano ya wananchi.

Aidha, wameeleza kuwa licha ya kubadili miradi ya maendeleo na kuielekeza tofauti wamesema pia amehujumu miradi ya maji katika kijiji hicho na bado imekuwa na changamoto kutokana na usimamizi mbovu wa kiongozi huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti, Josephati Kiluka amesema kuwa taarifa zilizotolewa na wananchi hao hazina ukweli wowote, na kusema miradi hiyo imeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na baadhi ya viongozi kuweka siasa kwenye miradi hiyo.

“Tatizo kubwa wanasiasa kwa sababu huwa wanaongea kuwafahadaa wananchi, lakini miradi mingi ya maendeleo imekwamba kutokana kuwekwa siasa, lakini hayo madai wanayotoa dhidi yangu si kweli.” Kiluka

Wagombea ubunge waingia mitini na fomu, msimamizi awataja
Viporo vya Simba vyaanza kuchacha, Muwa wagoma kuliwa