Kundi la Wanamgambo wa Al-Shabaab wamevamia jengo la Serikali Jijini Mogadishu na kuua watu takribani 11 akiwemo naibu waziri wa ajira.

Shambulio hilo la risasi lilitokea muda mfupi baada ya shambulio la kujitoa mhanga kwenye gari lililotokea karibu na jengo hilo.

Aidha, Al-Shabaab wamekiri kuhusika na shambulio hilo lililojeruhi watu wengine takribani 10. ambapo tukio hilo limetokea karibu sana na Makao Makuu ya Intelijensia ya nchi hiyo.

Shambulio kama hilo lilifanyika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu, ambapo takribani watu 24 walifariki, kabla ya hapo kulikuwa na milipuko miwili ya kujitoa mhanga.

Hata hivyo, Al- Shabaab ndicho kikundi hai zaidi cha wanamgambo wenye lengo la kuitoa Serikali ya Somalia inayopewa nguvu na mataifa ya Magharibi.

Waganga wa kienyeji wawekwa kikaangoni Sumbawanga
Habari Picha: Mwakinyo amchakaza Gonzalez raundi ya 5