Imeelezwa kuwa zaidi ya askari tisini wa jeshi la Chad wameuawa katika shambulio lililofanywa na wanamgambo wa Boko Haram.

Rais  wa nchi hiyo Idriss Deby amesema kuwa, shambulio hilo ni baya zaidi kuwahi kufanywa na wanamgambo hao wa Boko Haram katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Rais Deby ametembelea eneo lilipotokea shambulio hilo Magharibi mwa Chad, eneo lililopo kwenye mpaka wa nchi hiyo na nchi za Niger na Nigeria.

Mamia ya askari wa jeshi la Chad wameuawa tangu wanamgambo hao wa Boko Haram waanze mapigano katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Nigeria mwaka 2015, mapigano ambayo pia yamesababisha zaidi ya watu elfu moja kuyakimbia makazi yao.

Nchini Nigeria, Wanamgambo hao wa Boko Haram wamewaua askari  47 wa jeshi la nchi hiyo katika shambulio la kushtukiza lililotokea kwenye mji wa Maiduguri.

Saliboko ajiwekea malengo Lipuli FC
Senzo: Tutasajili kwa mapendekezo ya kocha