Mahakama nchini Libya imewahukumu kifo wanajeshi 45 baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya kuwaua watu kwa kuwafyatulia risasi mwaka 2011 wakati wa harakati za kumuondoa Madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.

Taarifa kutoka wizara ya sheria ya nchi hiyo imesema kuwa waliohukumiwa vifo hivyo ni wanajeshi ambao walikuwa watiifu kwa Gadafi na mauaji hayo yalifanyika katika wilaya ya Abu Slim kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.

Aidha, licha ya wanajeshi hao 45 kuhukumiwa kifo wengine 54 wamehukumiwa vifungo mbalimbali 22 wakiachiliwa huru na wengine watatu wakifa kabla ya hukumu kutolewa.

Hata hivyo, nchi Libya imekuwa na hali tete ya amani tangu Rais wa zamani wa nchi hiyo Muamar Gadafi apinduliwe na baadaye kuuawa ambapo kumekuwa na vikundi kadhaa vya waasi vimekuwa vikizipinga Serikali zinazokuwa madarakani.

Video: Lissu ainyooshea kidole Chadema, Mume amuua mke kwa mundu, auawa
Prof. Lipumba amtaka Maalim wayamalize