Serikali nchini Mali imesema, wanajeshi 53 na raia mmoja wameuawa katika shambulio la kigaidilililo tokea nchini humo.

Shambulio hilo linalosadikiwa kufanywa na wanamgambo wa Kiislamu, lilitokea jana Ijumaa kwenye kambi ya jeshi katika eneo la Indelimane lililo Kaskazini, mpakani mwa nchi hiyo na Niger.

Tukio la Ijumaa limejiri baada ya shambulio la awali la mwezi Oktoba, lililosababisha vifo vya wanajeshi 38 wa nchi hiyo.

Uingereza: Waziri Boris atengua kauli

Kwa muda mrefu sasa maeneo ya katikati pamoja na Kaskazini mwa nchi hiyo, yamekuwa yakikabiliwa na vurugu za mara kwa mara na mashambulizi baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2012.

Katika mapinduzi hayo waasi wanaotaka kujitenga pamoja na makundi yenye mafungamano na al-Qaeda yalianza kudhibiti eneo hilo.

 

Serikali yazindua 'App' yakubana Trafiki wala rushwa
Uingereza: Waziri Boris atengua kauli