Wanajeshi watano wa Nigeria wameuwawa na wengine 30 wametoweka kufuatia shambulizi lililofanywa na magaidi wa Boko Haram katika kambi ya wanajeshi hao.

Hayo yamejiri baada ya kufanyika kwa shambulio lililofanywa na magaidi katika kambi ya wanajeshi iliyopo mjini Maiduguri baada ya magaidi kufanikiwa kuiteka kambi hiyo.

Hadi kufika sasa bado hakuna taarifa zozote ambazo zimetolewa juu ya hatima ya wanajeshi hao walinda amani Nchini Nigeria waliotoweka.

Umoja wa mataifa (UN), umetangaza kuwa kufuatia kuongezeka kwa duru mpya ya mashambulio ya magaidi wa boko haram kaskazini mashariki mwa Nigeria, zaidi ya watu 30,000 katika eneo hilo wamelazimika kukimbia makazi yao na kuishi kama wakimbizi katika maeneo maengine ya nchi yao.

Ni miaka tisa sasa mapigano baina ya wanajeshi wa serikali ya Nigeria na magaidi yamekuwa yakiendelea, Zaidi ya watu 27,000 wameuwawa na wengine milioni 1.8 kuachwa bila makazi na kupelekea mgogoro mkubwa wa kibinadamu katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika.

Serikali kurasimisha ajira ya kuokota Makopo
Usafiri wakwamisha kesi ya Kisena na wenzake

Comments

comments