Jumla ya watu 9 wakiwemo Wanafunzi watano wa Shule ya Msingi Nyachilo, wameripotiwa kufariki dunia kufuatia mvua kubwa, zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Morogoro.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amesema watu hao wamekufa maji katika matukio tofauti na sehemu tofauti, ikiwemo wanafunzi watano kusombwa na maji katika Mto Mvuha, wakati wakitoka shuleni.

Watu wengine wawili wakielezwa kupoteza maisha baada ya kuzama katika Bwawa la kuhifadhia maji machafu ya miwa, linalomilikiwa na kiwanda cha Sukari cha Kilombero.

Kamanda Mutafungwa amewataja waliokufa katika matukio hayo kuwa ni Rajabu Issa, Shabani Msimbe,Neema Rajabu,  Latifa  Khalidi, Munira Khalid, Omary Khalidi ambao miili yao imepatikana huku mmoja wao Zainabu  Rajabu, mwili wake bado haujapatikana.

Aidha ametoa wito kwa wananchi, wazazi na walimu kuhakikisha wanakaa karibu na Watoto wao ili kuhakikisha wanakuwa salama kipindi hiki cha mvua.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 16, 2019
Pyramids Fc 'kuwaburuza' Yanga CAF