Wanafunzi Sita wa shule ya Sekondari ya Katoro Islamic Seminary, wanaotuhumiwa kwa kosa la mauaji ya mwananfunzi mwenzao aliyefahamika kwa jina la Mud Muswadiku wamefaulu vizuri mitihani yao ya kidato cha nne kwa kupata daraja la pili na la tatu licha ya kufanyia mtihani wao gerezani.

Ambapo Mkuu wa Gereza la Bukoba, Jasson Kaizilege amesema kuwa vijana wanne wamepata daraja la pili na vijana wawili wamepata daraja la tatu, hivyo ameongezea kuwa huenda vijan ahao wangepata ufaulu wa juu zaidi ya huo walioupata kama wasingefanya mtihani huo katika mazingira magumu.Aa

“Wawili wamepata Division 3, vijana wanne wamepata Division 2, sisi sote tumepata faraja kubwa na tukawa tunajiuliza, hawa vijana pengine wangekuwa nje wangefanya vizuri sana zaidi” amesema Mkuu wa Gereza.

Aidha, Kaizilege amesema kuwa baada ya kupata kibali kilichoruhusu wanafunzi hao kufanya mtihani katika gereza hilo, iliwabidi wawaandae watoto hao kisaikolojia mbali na kuandaa mazingira ya kufanyia mtihani.

Wanafunzi hao ni Husama Ramadhan, Sharif Huled , Hussein Mussa, Abdallah Juma, Sharif Amri na Fahad Abdulraziz, wanashtakiwa kwa kumuua mwanafunzi mwenzao Mud Muswadiku (19) kwa tuhuma za kujihusiha na mapenzi ya jinsia moja

Katika kosa walilotenda Aprili 14, 2019 la kumuua kwa makusudi mwanafunzi mwenzao hivyo wanakabiliwa na kesi ya mauaji namba 18/2019.

Kenyatta apangua safu ya Mawaziri
Tiketi za mabasi sasa kieletroniki

Comments

comments