Jumla ya wanafunzi 400 wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE) wamekubali kujitolea kufundisha shule mbalimbali za Manispaa ya Temeke.

Hayo yamesemwa katika semina ya maadili na miiko ya taaluma ya ualimu na mwanzilishi na mratibu wa zoezi hilo Mwl. Amijidius Cornel ambapo amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya nauli.

”Tuna changamoto zinazotukabili katika utekelezaji wa majukumu yetu haya ya kufundisha kwa kujitolea hivyo tunaomba serikali itufadhili nauli ili tuweze kuzifikia shule nyingi zaidi,” amesema Mwl. Cornel

Aidha, baada ya kupata semina kuhusu maadili ya ualimu, wamesema kuwa wamekamilika na wapo tayari kuitumikia elimu ambayo wameipata ili kujijenga na kupata uzoefu utakaowasaidia kuwa bora zaidi hata pindi watakapopata ajira rasmi.

Hata hivyo, muhula wa masomo kwa mwaka 2018 unatarajiwa kuanza rasmi Jumatatu ijayo, Januari 8 ambapo walimu hao wataanza kazi katika shule mbalimbali za Manispaa ya Temeke.

Video: Rais Magufuli asifu mchango wa Kingunge, Lissu alivyopaa dk 500 Ulaya
Magazeti ya Tanzania leo Januari 7, 2018