Mkufunzi msaidizi wa jeshi la akiba (mgambo), Said Athumani Ng’imba mwenye namba MG129191anatafutwa na jeshi la Polisi mkoani Singida kwa tuhuma ya kutoa adhabu kwa wanafunzi wawili watumbukie kwenye dimbwi na kusababisha vifo nyao.

Wanafunzi waliofariki dunia ni Emmanuel Hamis (20) mkazi wa kijiji cha Mudida na Ismael Hussein (22) mkazi wa kijiji cha sepuka.

Imeelezwa kuwa wanafunzi hao walikuwa wanahudhuria kozi ya mafunzo ya awali ya jeshi la akiba ambayo yanaendelea kufanika kijiji cha Mudida.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amethibitisha kutokea kwa tukio hilo siku ya Novemba 20, mwaka huu katika kijiji cha Mudida.

Amesema wanafunzi baada ya kutohudhuria vipidi vya mafunzo vya siku moja, Novemba 19 mwaka huu mkufunzi aliwapa adhabu ya kutumbukia kwenye dimbwi lililokuwa limejaa maji ambapo licha ya jitihada za uokoaji walipoteza maisha.

“Baada ya kutumbukia, walizama ndani ya dimbwi na hawakuonekana, kitendo hiki kilisababisha mkufunzi msaidizi kutimua kusikojulikana hadi sasa. Tayari tumeanza kumsaka kwa nguvu na tunatarajia muda si mrefu atakuwa mikononi mwetu” Alieleza Kamanda Njewike

Na kuongeza kuwa ” Jeshi la polisi lilishirikiana na jeshi la zimamoto na uokoaji, lililofanya juhudi kubwa kuwaokoa, liliwaopoa kutoka majini wakiwa tayari wamefariki dunia”.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio zimeeleza wanafunzi hao kabla ya kutumbukia walibebeshwa kila mmoja mfuko mgongoni uliojazwa mchanga.

LIVE Dodoma: Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi, ujenzi wa makao Makuu ya ulinzi wa Taifa
Mbunge Neema Mgaya ahitimisha ziara Njombe, akabidhi Saruji mifuko 150