Wanafunzi tisa wa Shule ya msingi ya St. Gabriel, Mwingi Kaunti ya  Kitui nchini Kenya, wamefariki huku wengine 32 wakiwa wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi ya shule na lori usiku wa kuamkia leo.

Wanafunzi nane wametajwa kufariki katika eneo la ajali hiyo huku mmoja ambaye anaongeza idadi ya kufika tisa amefariki akiwa hospitali ya taifa wakati anapatiwa matibabu.

Aidha, wanafunzi hao walikuwa wakitokea Mombasa katika safari ya kimasomo ambapo basi lao liligongana uso kwa uso na Lori katika daraja la Kanginga, Kilomita moja kutoka mji wa Mwingi kwenye barabara ya Thika-Garissa usiku wa manane.

Majeruhi 32 walofikishwa katika Hospitali ya Mwingi, wanafunzi Sita wanadaiwa kuwa katika hali mbaya (mmoja amefariki na kubaki watano)  ambapo wameshahamishwa katika hospitali ya Taifa ya Kenya, (Kenyatta National Hospital).

Hata hivyo, katika ujumbe wake kwa wazazi na walezi wa wanafunzi, Rais Kenyatta amesema ni bahati mbaya kwamba maisha ya wanafunzi wasio na hatia wamepotea huku taifa likiwategea kuwa viongozi wa hapo baadae.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 6, 2018
Wapinzani wasijisumbue, ushindi uko palepale- Nape Nnauye