Wanafunzi 101 mkoani Shinyanga wamepata ujauzito ndani ya mwezi mmoja kuanzia Machi hadi Aprili mwaka huu wakati wa likizo ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto la KIVULINI, Yassin Ally amesema mkoa huo Mbali na ujauzito, una kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni ukifuatiwa na Tabora.

Amesema, “Kwa mujibu wa taarifa za dawati la jinsia, Machi – Aprili wanafunzi 101 wameripotiwa kupata ujauzito, ambapo Halmashauri ya Shinyanga ina wanafunzi 26, Kishapu 25, Manispaa Shinyanga 20, Msalala 17 na Kahama 16”.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba amesema Serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobaInika kuwapa ujauzito wanafunzi hao.

Kisa Domayo, Zaka awatolea uvivu Simba SC
Ajira: Makampuni 10 yatangaza nafasi za kazi, ziko hapa