Klabu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam leo Jumapili Juni 10 imefanya mkutano huku moja kati ya Agenda za mkutano huo ikiwa ni kujadili kujiuzulu kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji.

Katika mkutano huo wanachama wamekataa kuridhia kujiuzulu kwa mwenyekiti wao Yusuph Manji wakisema hawatambui kujiuzulu kwa mwenyekiti huyo na bado wanamtambua kama mwenyekiti wao.

Aidha kupitia mkutano huo wanachama wameridhia kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu na kuunda kuunda kamati ya mpito itakayosimamia maswala yote ya kifedha ndani ya timu hiyo ikiwemo usajili.

Kamati hiyo ipo chini ya Mwenyekiti, Abbas Tarimba katibu ni Said Meck Sadick huku wajumbe wakiwa ni Abdallah Binkleb, Nyika Hussein, Mashauri Lucas, Yusyphed Muhandeni, Hamad Islam, Makaga Yanga, Ridhiwani Kikwete na Hussein Ndama.

Video: Terrence ‘ampasua’ aliyempiga Manny Pacquiao
Mwenyekiti UVCCM apata ajali