Jeshi la Polisi mkoani Mwanza lina washikilia wapenzi wawili kwa tuhuma za kumuua mtoto wa miezi 9 kwa kumnyonya kwa kanga ili wafunge ndoa.

Helena Washera (19), mama wa mtoto huyo anadaiwa kuwa ndiye aliyetekeleza mauaji hayo kwa kutumia kanga.

Polisi wamesema mpenzi wake, Lucas Jackson (24) alimlaghai kufanya kitendo hicho ili amuoe. Baada ya kumuua mwanaye Helena na Lucas waliendelea na mahusiano bila kuoana.

Baba wa mtoto, James Simon alitoa taarifa Polisi baada ya kutomuona mwanaye kwa muda na alipomuuliza Mama yake alidai yupo kwa Bibi lakini hata alipoenda huko hakumuona.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jumanne Muliro amesema baada ya kuhojiwa wawili hao walikiri kufanya mauaji hayo.

Mifupa inayodhaniwa kuwa ni ya mtoto huyo imepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi.

Rais Putin asaini katiba inayombakiza madarakani
Maalim Seif achaguliwa kuwa Mwenyekiti ACT - Wazalendo

Comments

comments