Wanariadha wawili wa Kenya, wamefanyiwa vipimo na kukutwa na chembe chembe dawa za kusisimua misuli huko mjini Beijing nchini China inapofanyika michuano ya dunia.

Joyce Zakary na Koki Manunga walifanyia vipimo mara baada ya kufanya vizuri katika mbio za mita 400 hatua ya mchujo na walitarajiwa kupambana na washiriki wengine kutoka dunaini katika mchezo wa hatua ya nusu fainali.

Shirikisho la riadha duniani IAAF, limethibitisha taarifa hizo, na tayari wawili hao wameshaondolewa kwenye mlolongo wa washindani huko mjini Beijing, nchini China.

Wanariadha hao wanasubiri kutangazwa kwa adhabu ya kufungiwa kujihusisha na mchezo wa riadha duniani kote ambayo inatarajiwa kuwa zaidi ya mwaka mmoja.

Zakary alikuwa sehemu ya waliofanya vyema katika mbio za mita 400 mwanzoni mwa juma hili na kutinga kwenye hatua ya nusu fainali, lakini dakika chache baadae alifuatwa na kufanyiwa vipimo na ndipo alipokutwa na chembe chembe hizo.

Manunga alipambana na wenzake katika mbio za mita 400 siku ya jumapili.

Serikali Yakataa Ombi La UKAWA Kutumia Uwanja Wa Jangwani Jumamosi Hii
Dibaba Atwaa Medali Ya Dunia mita 1500