Wananchi wa Kata ya Mabilioni Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kutumia maji ya Mto Ruvu yaliyopimwa na kugundulika kuwa na chembe chembe za Kinyesi cha Binadamu.
 
Hayo yamesemwa na Afisa Elimu wa Kata ya Mabilioni, Richard Sekibojo alipokuwa akitoa taarifa kwa mkuu wa wilaya ya Same, Rosemery Sitaki.
 
Amesema kuwa wakazi 5109 wanaounda kaya 1158 wamekuwa wakitumia maji ya Mto Ruvu unaopita katika vijiji vitatu viliyoko katika Kata hiyo vya Chekereni, Mabilioni na Ruvu Mbuyuni kwa ajili ya Kunywa, Kupikia pamoja na Kilimo .
  • Picha: Rais Magufuli akutana na Bill Gates Ikulu Dar es salaam
 
“Mkuu wa wilaya, Kata ya Mabilioni haina maji safi ya kunywa,kwani wananchi wanatumia maji ya Mto Ruvu kwa matumizi yote ya nyumbani pamoja na Kilimo na maji hayo yalipimwa yakaonekana kuwa yana chembechembe za kinyesi cha binadamu zinazosababisha ugonjwa wa kipindu pindu,”amesema Sekibojo.
 
  • Video: Majaliwa ampa siku 15 mweka hazina Sikonge
 
Hata hivyo, Mkuu wa wilaya hiyo amesema kuwa upo mradi mkubwa wa maji wa serikali toka wizara ya Maji ambao utaanza kutoa maji katika Bwawa la Nyumba ya Mungu kupitia wilaya ya Mwanga, Same hadi Korogwe mkoani Tanga

Video: Lowassa achekelea, Waziri akwepa kutumbuliwa
Video: Amber Lulu afunguka uhusiano wake na Harmorapa na jinsi ulivyoanza