Wakala wa Serikali Mtandao umetengeneza Mfumo Shirikishi wa Kusimamia Shughuli na Rasilimali za Taasisi (ERMS) utakaowezesha kusimamia, kufuatilia, kukagua na tathmini ya utekelezaji wa shughuli zote za umma kwa ufanisi.
 
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala, Dkt. Jabiri Bakari wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa matumizi ya tehama katika kuboresha utendajikazi serikalini.
 
Amesema kuwa wameamua kutumia utaalamu wa kidigitali kutengeneza mfumo wa ERMS ambao ni dirisha moja linalounganisha shughuli zote za ndani ya taasisi kuongeza ufanisi katika utendajikazi na utoaji huduma bora kwa umma.
 
Aidha amesema kuwa kuwa mfumo huo utakuwa na moduli 18 zinazounganisha shughuli mbalimbali za utendajikazi zinazotegemeana kuwezesha kubadilisha taarifa miongoni mwa idara na kusimamia rasilimali watu, fedha na vitendea kazi.
 
Dkt. Bakari amesisitiza kuwa mfumo huo unawezesha ushughulikiaji wa miamala kutoka idara moja hadi nyingine zikiwemo ankara za bidhaa na huduma, mapato na matumizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa shughuli kulingana na mipango na bajeti.
 
“Pia utawezesha usimamizi wa majukumu ya watumishi, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi, utekelezaji wa shughuli za manunuzi na utayarishaji wa taarifa mbalimbali za utendaji”amesema Dkt. Bakari
 
Hata hivyo amesema kuwa mfumo huu utawawezesha maofisa masuuli na watumiaji wengine wa mfumo kupata taarifa mbalimbali kulingana na mahitaji yao.

Video: Masanja ameachia ngoma yake mpya ''Nii'', Itazame
Mchungaji aua waumini kwa kuwanywesha JIK