Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara leo katika kikao cha kuwapokea wanachama wapya kutoka vyama vya siasa mbalimbali ili kujiunga na Chama cha mapinduzi kilichofanyikia ndani ya ukumbi wa CCM  wilaya Tarime, amekemea baadhi ya wanasiasa kutumia nafasi ya ugonjwa wa Corona kupuuza maelekezo yaliyotolewa na wizara ya Afya.

Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kuwaonya baadhi ya waendesha vyombo vya moto hususani waendesha pikipiki wa mipakani kama vile mpaka wa Sirari kuwapakia na kuwavusha wageni kutoka nchi jirani ya Kenya usiku kuingia Tanzania bila kupitia eneo maalumu la mpakani ili kujulikana na kufanyiwa  uchunguzi wa vipimo kama wanamaambukizi ya virusi vya Corona.

”Sasa hivi kuna ugonjwa wa Corona(Cocid19) na serikali imetoa taarifa kwa wananchi wake kujikinga na maambukizi kwa hali hiyo asiwepo mtu wa kupuuza maelekezo ya wataalamu wa Afya kwani kuzingatia kuwa Tarime ipo mpakani mwa nchi jirani ya Kenya na isitokee mwanasiasa anatumia nafasi hiyo kuwapotosha wananchi na waendesha Bodaboda wanaowapakia watu na kuwavusha mpaka bila kufuata utaratibu wa serikali” amesema Waitara

Kwa upande wake katibu  wa Chama cha mapinduzi wilaya Tarime, Khamisi Mkaruka amesema kuwa leo wamepokea wanachama wapya 55 kutoka vyama vya upinzani  wakiongozwa na mwenyekiti wa Chama cha Demokorasia na maendeleo wilaya ya Tarime Mwita Joseph.

IMF: Corona imetikisa uchumi wa Dunia
Masauni : mahabusi wapewe dhamana nchi nzima kukinga Corona

Comments

comments