Mwezi mtukufu wa Ramadhan umeanza kwa Waislam wapatao bilioni moja, milioni mia sita duniani kote, ambapo inawabidi kutekeleza ibada na kufunga kuanzia alfajiri hadi magharibi na baada ya hapo hujumuika pamoja kwa chakula cha jioni “Iftar”.

Ramadhan huanza mwezi wa tisa wa kalenda ya Ki-Islam ambapo Waislam wanaamini Kuran Takatifu iliwasilishwa kwa Mtume Mohammad katika karne ya saba.

Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Waislamu wanatarajiwa kuwa wakarimu kwa kuwasiadia watu wasiojiweza

Aidha, ndani ya mwezi huu mtukufu kuna siku 10 za mwisho za kukamilisha mfungo ambazo zinachukuliwa kuwa siku Takatifu zaidi ambazo watu hulala kwenye misitiki wakitafuta neema zaidi ya mwenyezi Mungu katika masiku yanayotoa siku maalumu iitwayo “Lailatul Kadri” usiku mtukufu wa mwaka kwa kalenda ya ki-Islam.

Dar24 Media tunawatakia Waislamu wote Ramadhan Kareem.

LIVE: Mwili wa Dkt. Reginald Mengi ukiagwa wakati huu Karimjee
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 7, 2019

Comments

comments