Leo Septemba 30, Rais Magufuli amepokea taarifa kuhusu ushauri alioutoa juu ya kuwasamehe washtakiwa walio uhujumu uchumi wa nchi na wapo tayari kutubu na kurejesha fedha na mali walizohujumu ambapo taarifa hiyo imeripotiwa na Mkurugenzi wa Mashataka DPP, Biswalo Mganga ambaye ametangaza jumla ya washtakiwa 467 wapo tayari kurudisha jumla ya shilingi Bilioni 107 na zaidi.

”Katika kipindi hiki ofisi yangu imepokea barua za washtakiwa 467 wa kesi za uhujumu uchumi wanaomba kukiri makosa yao na kurejesha fedha walizowaibia watanzania” amesema DPP Mganga.

Katika taarifa hiyo amesema kuna makundi mawili ambapo, kundi la kwanza ni wale washtakiwa ambao wapo tayari kurudisha fedha muda wowote kuanzia sasa hivi kwa shilingi na dola, lakini pia lipo kundi la washtakiwa waliotayari kurudisha fedha kwa awamu kadri watakavyokubaliana kwa mujibu wa sheria.

Ambapo jumla ya shilingi Bilioni 7, dola 2,523,704.58 sawa na bilioni 5  zipo tayari kurudisha wakati wowote kuanzia hivi sasa, huku bilioni 94 zipo tayari kulipwa kwa awamu.

”Mhe Rais kati ya washtakiwa hao jumla ya shilingi bilion 7, 884, 901, 526 wapo tayari kurudisha muda wowote hata sasaivi, washtakiwa wengine ambao wapo tayari kurudisha wao kesi zao zipo kwenye dola, dola 2,523,704.58 sawa na bilioni 5 na milioni 717, wapo tayari kurudisha” amesema Mganga.

Hatua hiyo ni kufuatia ushauri alioutoa rais Magufuli Septemba 22, 2019 wakati akiwaapisha baadhi ya viongozi aliowachagua ambapo alitoa siku 7 kwa Mkurugenzi wa mashtaka kutoa ruhusa kwa washtakiwa wa makosa ya uhujumu uchumi kutubu na kurudisha fedha zote wanazodaiwa.

Aidha baadhi ya wananchi waliokuwa wanafuatilia kipindi hiko ambacho kilikuwa kinarushwa mubashara katika runinga na baadhi ya mitandao ya kijamii wamepongeza na kusifia juhudi na jitihada za rais Magufuli katika kufanya makusanyo ya fedha za nchi.

Rais Magufuli aonya, aongeza siku 7 za msamaha watuhumiwa uhujumu uchumi
Amuua baba, mama na kaka yake kisa mpenzi wa Twitter