Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wamepigwa msasa kuhusu maambukizi ya VVU na Ukimwi ambapo semina hiyo imeandaliwa na Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS  kwaajili ya kutoa habari makini zinazohusu Ukimwi.

Semina hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma ambapo wahariri hao wamejifunza mambo mengi kuhusu utoaji wa elimu ya maambukizo ya ukimwi.

Aidha, miongoni mwa masuala yaliyozungumzwa katika semina hiyo ni changamoto mbalimbali zinazoikabili Tanzania katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.

Hata hivyo, katika semina hiyo zimeanishwa changamoto ambazo zimekuwa zikiikabili jamii ambayo imekuwa ikiathirika na tatizo hilo kuwa ni pamoja na Sheria ya Magereza, adhabu ndogo kwa wanaoambukiza watu wengine VVU kwa makusudi zilizoanishwa katika Sheria ya Ukimwi, mila potofu na desturi zilizopitwa na wakati (ukiwamo ukeketaji) na unyanyasaji wa kijinsia.

Video: Siri nzito kung'oka kwa IGP Mangu, Prof. Kabudi, Simbachawene watajwa kumrithi Muhongo
Magazeti ya Tanzania leo Mei 29, 2017

Comments

comments