Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wenye virusi vya Corona imeongezeka nchini na kufikia sita ambapo wagonjwa wawili wamegundulika Dar es Salaam hivyo kufanya idadi ya wagonjwa waliothibitika nchini kuongezeka.

Hata hivyo taarifa kutoka Wizara ya afya inasema kuwa Mgonjwa wa kwanza alisafiri katika mataifa ya Uswiss, Denmark na Ufaransa kati ya tarehe 5 na 13 Machi na kurejea nchini tarehe 14 Machi 2020.

Mgonjwa wa pili alisafiri nchini kuelekea Afrika akusini baina ya tarehe 14 na 16 Machi na kurudi nchini Tanzania tarehe 17 Machi 2020.

Kwamujibu wa Wizara ya afya wagonjwa hao wote wawili wametengwa huku maafisa wanashughulika kuwatambua watu wengine 46 mkoani Arusha  na wengine 66 walioko Dar es Salaam waliokua karibu na wagonjwa waliothibitika kuwa na Covid-19

Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu kadri wanavyopokea taarifa na elimu za mara kwa mara kwa njia mbalimbali.

 

CORONA yasitisha Copa Libertadores, Copa Sudamericana
Noti ya Tanzania haibebi vimelea vya Virusi