Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI imeanzisha huduma ya kutoa dawa za usingizi (Reginal block Anaesthesia) ambapo eneo husika linalofanyiwa upasuaji ndilo litakalo husika kwa kuzuia mishipa ya fahamu na hivyo mgonjwa kuwa macho na kuzungumza au hata kusoma gazeti.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt Respicious Boniface katika hafla ya kuwapokea wakufunzi wawili kutoka Chuo kikuu cha Latvia cha nchini Latvia ambao watatoa mafunzo hayo ya kibingwa ya kuzuia mishipa ya fahamu katika eneo linalofanyiwa upasuaji badala ya kumlaza mgonjwa usingizi (Nusu kaputi) kwa zaidi ya siku kumi kwa madaktari bingwa wa MOI na madaktari walio mafunzoni

“Huu ni muendelezo wa mafunzo ambayo tulishayaanzisha kwa mdakatari wetu , lengo kubwa la mafunzo haya na ujio wa wakufunzi hawa ni kuhakikisha huduma hii inaendelea kutolewa hapa MOI. Ni mbinu bora na salama ya kumlaza mgonjwa kwaajili ya upasuaji ambapo mgonjwa anaweza kufanyiwa upasuaji huku anasoma kitabu (Novel) ambapo baada ya upasuaji mgonjwa hapati maumivu makali na anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani siku hiyohiyo” alisema Dkt Boniface

Amesema kuwa pamoja na wakufunzi hawa kutoa mafunzo, Taasisi ya MOI itasaini mkataba wa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Latvia lengo kuu ikiwa ni kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma za kibingwa za Usingizi (Anaesthesia)

Aidha, Dkt Boniface ameongeza kwamba kwa sasa Taasisi ya MOI imeanzisha huduma ya kulazwa na kufanyiwa upasuaji siku hiyo hiyo yaani (Same day Surgery) hivyo huduma hii itatumika katika wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji na kuruhusiwa kwani wagonjwa hawapati maumivu makali baada ya upasuaji na hakuna masharti magumu baada kufanyiwa upasuaji

Kwa upande wake Profesa, Alex Miscuks kutoka Chuo Kikuu cha Latvia amesema kuwa ni heshima kubwa kupata fursa ya kuja kubadilishana uzoefu hapa Tanzania kwani pamoja na kutoa mafunzo atapata fursa ya kujifunza mambo mengi.

Naye Dkt. Iveta Gobovska ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha wagonja mahututi katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Latvia amesema amefarijika kupata fursa ya kuja kubadilishana uzoefu na madaktari wa Tanzania na anamini pande zote mbili zitanufaika na mafunzo haya.

LIVE: Rais Magufuli akizungumza na Wachimbaji, Wafanyabiasha na Wadau wa Sekta ya Madini
Video: Lissu asubiri muziki wangu - Ndugai, Adaiwa kumuua mdogo wake kisa mgawo kishika uchumba

Comments

comments