Wafungwa na idara ya wafungwa nchini Kenya wameshikana mashati mahakamani kuhusu mgogoro wa nyongeza ya mshahara wao wa sh.0.20 kila siku mbali na kulipwa bila kucheleweshwa.

Malipo hayo yaliangaziwa 1979 licha ya kuongezeka kwa gharama ya kuishi.

Mawakili wa wafungwa hao wamewasilisha kesi mahakamani wakitaka kuaziwa upya kwa malipo hayo.

Wafungwa hao wanapigania kuongezwa kwa dola senti moja kwa wiki wanayolipwa kwa sasa.

Nicholas Ouma Obonyo na Samuel Ng’ondo walisema kuwa kamishna wa jela nchini Kenya alishindwa kuwalipa licha ya kupata agizo kutoka kwa wizara ya fedha.

Kifungu cha tano cha shirika la huduma za wafungwa nchini Kenya inasema kuwa viwango vya mapato vitakuwa senti 20 kwa wafungwa waliopo katika gredi A, 15 kwa aliyepo katika gredi B na senti 10 kwa mfungwa aliyepo katika gredi C.

Lakini akizungumza mahakamani kamishna jenerali alisema kuwa hana uwezo wa kubadilisha sheria iliopo kwa kuwa malipo hayo yapo katika sheria ya Kenya.

Aliongezea kuwa walalamishi hawafanyi kazi ya kuajiriwa ambapo mshahara unatakiwa kuwa sawa hivyobasi madai yao ya kudai kufanywa watumwa hayapo na sio ya haki.

Afisa huyo wa magereza anasisitiza kuwa wafungwa wanatakiwa kufanya kazi chini ya sheria.

”Lengo la kuwapatia kazi wafungwa ni kuwapatia ujuzi na elimu kupitia mafunzo ili kuwawezesha kuingiliana na jamii wakati wanapoachiliwa”, anasema.

Msiponilipa mshahara wangu nawashtaki- Lissu
Wachimbaji wa dhahabu Namungo wapewa somo, 'Tunzeni mazingira'