Rais wa Shirikisho la Mpira Nchini Kenya (FKF), Nick Mwendwa amesema kuwa kujiondoa kwa baadhi ya wadhamini waliokuwa wakidhamini ligi hiyo kumelifanya soka la nchi hiyo kuanza kuyumba.

Amesema kuwa kujiondoa kwa wadhamini hao kutasababisha ligi hiyo kusuasua hivyo kuiathiri timu ya taifa ya nchi hiyo.

Aidha, Mwandishi wa habari wa gazeti la The Nation, David Kalimwa amezungumzia hali ya soka nchini humo baada ya baadhi ya makampuni kujiondoa kudhamini ligi hiyo.

“Hali ni ya wasiwasi kwa upande wa shirikisho la soka hapa nchini (FKF), wanajiuliza ni jinsi gani wataweza kuendesha ligi bila wadhamini, SportPesa wamejiondoa, baadhi ya makampuni nayo yamejiondoa hata kudhamini vilabu kama AFC Leopard na Gor Mahia ambavyo vinashiriki mashindano makubwa Afrika,”amesema Kalimwa.

Hata hivyo, sababu kubwa inayotajwa kusababisha kujiondoa kwa wadhamini hao ni serikali kuyapandishia kodi makampuni hayo, huku SportPesa ikijiondoa hata kumlipa kocha wa timu ya taifa hilo.

“

Sababu 3 Sugu kumkataa hakimu kuendesha kesi yake
Amuua mpenzi wake kisha aandika ujumbe mzito